Thursday, 14 July 2016

ENDA NASI LYRICS BY REUBEN KIGAME


Verse 1
Tunaomba uwepo wako uende nasi
Ewe Bwana wa majeshi utusikie
Kama huendi nasi, hatutaki kutoka hapa
Hatuwezi pekee yetu, enda nasi



Tu watu wa shingo ngumu tusamehe
Hatufai mbele zako, turehemu
Tusafishe ee Baba, tuonyeshe uso wako
Twahitaji neema yako, enda nasi



CHORUS

Tutavua mapambo yetu
Na vitu vyote vya thamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi

Verse 2
Tunaomba utuonyeshe njia zako
Kwa maana umetuita kwa jina
Twalilia Ee Bwana, utukufu na uso wako
Bila wewe tutashindwa, enda nasi



CHORUS
Tutavua mapambo yetu
Na vitu vyote vya thamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi

No comments:

Post a Comment